Gumzo Kuu
Loading...

Jinsi Ya Kushusha Video Kutoka Youtube Bila Ya Kutumia Programu Yeyote!

...Good News, Like Us Now.

Leo tunakuletea njia rahisi sana ya kuweza kushusha video hizo. Njia hii haitahusisha utumiaji wa programu nyingine yeyote.
Kabla sijakupeleka kwenye njia hiyo cha msingi ni kwamba uhakikishe tuu kwamba intaneti yako inakasi (ili video unayoishusha isije ikafeli kabla bado haijashuka yote).
Tuifahamu NJia Hiyo.
MUHIMU: Njia hii inakubali kwa watumiaji wa simu janja (Android tuu, simu zingine labda kujaribu) na kompyuta!.
HATUA 1: Fungua Video unayotaka kuishusha.



Ingia Katika Video Unayotaka Kuishusha

Mfano: 
HATUA 2: Ukurasa wa video ukishafunguka nenda katika eneo la URL naa baada ya WWW. Weka SS na kisha bofya Enter kwa watumiajia wa kompyuta na baada ya M. weka SS kwa watumiaji wa simu janja.



Weka SS Baada Ya WWW. Au M.

HATUA 3: Ukurasa mwingine utafunguka ukiwa na sehemu ya kushusha video hiyo. Kabla ya kuishusha unaweza ukachagua video hiyo iwe katika mfumo gani (mf MP4, 3GP n.k).



Chagua Aina Ya Mfumo Wa Video

HATUA 4: ukishamaliza chagua mfumo unaoutaka kisha chagua Download.



Baada Ya Kuchagua Aina Ya Mfumo Unachagua 'Download'
Baada Ya Kuchagua Aina Ya Mfumo Unachagua ‘Download’

Hongera mpaka sasa una uwezo wa kushusha video za Youtube moja kwa moja katika kifaa chako kwa mtelezo kabisa. Ningependa kusikia kutoka kwako hii imekaaje? Je kwako imekubali?.


UNA MAONI GANI KUHUSU HABARI HII

© Copyright TANYUZI (Tz-News)
Back To Top