Gumzo Kuu
Loading...

Jinsi Ya Kushusha Video Kutoka Youtube Bila Ya Kutumia Programu Yeyote!

Leo tunakuletea njia rahisi sana ya kuweza kushusha video hizo. Njia hii haitahusisha utumiaji wa programu nyingine yeyote.
Kabla sijakupeleka kwenye njia hiyo cha msingi ni kwamba uhakikishe tuu kwamba intaneti yako inakasi (ili video unayoishusha isije ikafeli kabla bado haijashuka yote).
Tuifahamu NJia Hiyo.
MUHIMU: Njia hii inakubali kwa watumiaji wa simu janja (Android tuu, simu zingine labda kujaribu) na kompyuta!.
HATUA 1: Fungua Video unayotaka kuishusha.



Ingia Katika Video Unayotaka Kuishusha

Mfano: 
HATUA 2: Ukurasa wa video ukishafunguka nenda katika eneo la URL naa baada ya WWW. Weka SS na kisha bofya Enter kwa watumiajia wa kompyuta na baada ya M. weka SS kwa watumiaji wa simu janja.



Weka SS Baada Ya WWW. Au M.

HATUA 3: Ukurasa mwingine utafunguka ukiwa na sehemu ya kushusha video hiyo. Kabla ya kuishusha unaweza ukachagua video hiyo iwe katika mfumo gani (mf MP4, 3GP n.k).



Chagua Aina Ya Mfumo Wa Video

HATUA 4: ukishamaliza chagua mfumo unaoutaka kisha chagua Download.



Baada Ya Kuchagua Aina Ya Mfumo Unachagua 'Download'
Baada Ya Kuchagua Aina Ya Mfumo Unachagua ‘Download’

Hongera mpaka sasa una uwezo wa kushusha video za Youtube moja kwa moja katika kifaa chako kwa mtelezo kabisa. Ningependa kusikia kutoka kwako hii imekaaje? Je kwako imekubali?.


HAYA HAPA MAMBO 10 YAKUZINGATIA KUHUSU KOMPYUTA.

Bila shaka umewahi kufika dukani kutazama kompyuta  ukashindwa uchague ipi?. Pengine umewahi kuchagua mashine kadhaa na ukashindwa ununue ipi? . Na hata baada ya  kununua kifaa hiki umekutwa na hisia za kutaka kuuza?. Kama haitoshi , baada ya kuuza umebaki njia panda kwa maswali mengi,  utachukua tena kompyuta ya sifa gani?.Usiumize kichwa .Haya maswali na mengine mengi ni jambo la kawaida  hasa kwa watumiaji wengi wa kompyuta, huu ni wakati  wa changamoto kama ilivyo katika kuchagua bidhaa ya aina yeyote ile . Linapokuja swala  la sifa zipi ni bora na  zipi sio bora, unapohitaji kuchukua, kuchagua , kupendekeza ama kununua kompyuta . Mtumiaji anapaswa kuwa na mwanga halikadharika elimu kiasi ,kuhusu tabia na uimara wa hiki chombo cha umeme . Hivyo kabla ya uamuzi wa kuchukua, kuchagua ,kupendekeza ama kununua kompyuta husika,inakupasa uwe na ujuzi na uelewa wa kutosha juu ya hiki chombo. Katika kukujuza zaidi juu ya sifa, tabia na uimara wa kifaa hiki cha digitali, Kitabukwanza inakuletea mambo 10 muhimu ya kuzingatia unapohitaji kompyuta .

...Fursa 10 Bora Za Ajira,Bofya Hapa Chini Kuziona.
1.Unapaswa kujua jina la kompyuta



2.Unapaswa kubainisha aina ya matumizi (elimu/mchanganyiko/mengineyo)


3.Unataka mashine ya ukubwa wa kiasi gani(Local disk)




4.Unahitaji kompyuta yenye kuchakata kwa uwezo gani(Processor)


5.Uwezo wa kompyuta kurejea kumbukumbu  ulizo tia ndani(RAM)






6.Ukubwa wa kioo(screen resolution) ni muhimu kwa watazamaji wa filamu''movies''






7.Unataka aina gani ya mfumo wa kuendeshea kompyuta  (window xp,vista,7,8,mac)


8.Inaandika/inachoma mfumo gani wa santuri(cd/vcd/dvd writer)




9.kamera(web cam)ni muhimu kwa mitandao ya kijamii,skype,facebook n.k


10.Ukubwa/umbo(size) 








PLAY VIDEO BELOW.

MAGU ON NEW ERA


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa mara ya kwanza amekutana na kuzungumza na wajumbe wa Sekretarieti ya chama hicho.

Magufuli pia amekutana na  wafanyakazi wa CCM Makao Makuu katika Ofisi za Chama hicho Mjini Dodoma ikiwa ni siku tano tangu achaguliwe kuwa Mwenyekiti wa Tano wa Chama hicho.

Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amekutana na watendaji hao wa CCM kwa lengo la kuwasalimia, kupokea maoni na ushauri wao juu ya utendaji kazi ndani ya Chama.

Katika mazungumzo hayo, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewapongeza watendaji wote wa Chama Cha Mapinduzi kwa kazi kubwa wanayoifanya na kwa namna ya pekee kwa jinsi walivyotoa mchango mkubwa kuhakikisha CCM inapata ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Pia amewataka kuendelea kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kwa lengo la kuendelea kukiimarisha Chama hicho ambacho kimebeba dhamana ya kuongoza Serikali kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Dkt. Magufuli amewahakikishia kuwa chini ya uongozi wake atafanyia kazi changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi wa CCM ikiwemo maslahi duni, vitendea kazi na kuondoa utegemezi.

Aidha, Dkt. Magufuli amewataka watumishi wa chama kutoa ushirikiano katika zoezi la uhakiki wa mali za Chama litakalosimamiwa na sekretarieti ya chama na ameahidi kuwa atahakikisha mapato yatokanayo na vyanzo vya mapato vya chama yanatumika ipasavyo.

Kwa upande wao watumishi wa CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Ndugu Abdulrahaman Kinana wamempongeza Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuchaguliwa kwa asilimia mia moja na wajumbe wa Mkutano Mkuu uliofanyika tarehe 23 Julai, 2016 Mjini Dodoma kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa.

Watumishi hao wamemuahidi kuendeleza utumishi uliotukuka na wameelezea matumaini yao ya kuboreshewa maslahi.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
© Copyright TANYUZI (Tz-News)
Back To Top