Gumzo Kuu
Loading...

MAJIBU MAZITO KWA MTATIRO..!!

...Good News, Like Us Now.

 Hoja hii hapa https://m.facebook.com/story.php… ya Kaka yangu Mtatiro ndio inayojibiwa, nimechukua kipande kidogo tu alichoishambulia ACT kuwa imekuwa kikwazo kwa ushindi wa UKAWA na kushindwa kutuwekea tafiti anayosema CUF ilibebwa na CHADEMA katika uchaguzi Mkuu wa 2015.
Aise my braza Mtatiro yaani sijaona analysis uliyofanya zaidi ya kuonesha vituko hebu niambie ACT unasema iliharibu Mpango wa UKAWA kwani ACT ilikuwa kwenye mpango wenu? Badala useme CHADEMA iliharibu ushindi wa UKawa segerea unalia na ACT Ambayo haikuwa kwenye mpango wenu.
Tuzungumzie JIMBO la Kasulu Mjini ulilolitolea matokeo kama mfano CCM kumshinda mgombea wa ACT kwa kura 3000 na kura hizo 3000 na kitu kuchukuliwa na UKawa, kama dhamira ni kuitoa CCM Huoni huyo mgombea wa UKAWA ndio aliharibu ushindi wa ACT kwa kuzipokonya kura 3000 za ACT ambazo zingeishinda CCM?
UKAWA Mngekuwa na dhamira ya kweli ya kuitoa CCM mngeijibu barua ya ACTwazalendo ya maombi yao ya kujiunga UKawa. Shida nyie mnaojiita upinzani mnaongozwa na chuki na ubinafsi mkiendelea hivi tusitegemee mabadiliko yeyote zaidi ya kuzidi kuua upinzani kwa kuchochoea migogoro. Tujifunze kwa wenzetu Afrika na Dunia wanaungana kuunganisha nguvu kukitoa Chama tawala nyie mnafikiria wengine wawaunge nyie tu hata kama hawafaidiki na muunganiko huo na wala hamuwahitaji mnataka wawafuate tu bila kujua hata malengo yenu ni yapi, na wanaowafuata kesho mnawasimanga mmewabeba.
My braza Julius S. Mtatiro tulipata uhuru ili kuuondoa utumwa Ila kijana kama wewe uliyeenda shule bado unawaza kitumwa kweli? kuwa eti ushindi wa CUF ni nguvu ya CHADEMA na sio nguvu ya ushirikiano UKAWA halafu cha kuchekesha unajichanganya tena kuwa NCCR NA NLD hawakuwa na ujenzi mzuri wa kujenga base za Chama chao na wagombea wao ndio maana CHADEMA ilishindwa kuwabeba.
Naomba nikuachie homework hizo base zilizojengeka za hivyo vyama viwili ndani ya UKAWA (CUF na CHADEMA) Vilijengwa wakati gani na Chini ya viongozi gani??
Jenga hoja kikubwa kamwe huwa halaumiwi mtu au taasisi ambayo haipo kwenye mpango wako au wenu wala hamna makubaliano yeyote, ACT haikuwa na makubaliano yeyote na UKAWA mlaumiane UKAWA wenyewe na sio ACTWAZALENDO.
Mwisho nakubaliana na hoja inayosema 'Tanzania kusoma ni kupata Sifa tu na sio kuelemika'

UNA MAONI GANI KUHUSU HABARI HII

© Copyright TANYUZI (Tz-News)
Back To Top